Makumbusho ya kale, Kwihara

| No comment yet
Elisante John na Simon Kabendera, Tabora
Januari 26,2012.

 

Mhifadhi msaidizi mwangalizi eneo la Kwihara, bw. Hamia Mohammed Kaloka,akiwaonyesha waandishi sehemu ya magazeti ya kale yaliyohifadhiwa kwenye tembe la Dk. Livingstone.

 

Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Singida na Tabora waliohudhuria mafunzo ya siku nne juu ya uandishi kwa njia ya mtandao, wakishuhudia kaburi la mwandishi John Shaw, aliyefariki dunia Mwaka 1871, wakati anamtafuta Dk. Livingstone.


WAANDISHI wa habari, wametakiwa kuyatangaza kikamilifu
maeneo mbalimbali ya makumbusho Mkoani Tabora, ili yawe kivutio ndani
na nje ya nchi na hivyo kuongeza pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Muungano wa vilabu vya habari nchini (UTPC), Abubakar
Karsan, alisema hayo, kwenye ziara ya mafunzo ya wanahabari wa mikoa
ya Singida na Tabora, waliozulu  tembe la Dk. Livingstone na makazi ya
mtemi Fundikira, yaliyopo Kwihara,Mjini Tabora.

Tembe hilo, lilikuwa kituo kikuu cha misafara ya watumwa, kutoka mikoa
ya magharibi mwa Tanzania na nchi jirani, wakati makazi ya mtemi
Fundikira ni ya kihistoria kwa utawala wa Unyanyembe, Mkoani Tabora.

Kutokana na hali hiyo, Karsan alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa
Wanahabari, kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutangaza
makumbusho hayo, ili yafahamike vizuri ndani na nje ya nchi, kwa ajili
ya kujipatia fedha za kigeni.

Licha ya kuzulu tembe na makazi ya mtemi Fundikira, pia waandishi
walitpata fursa ya kutembelea jiwe maarufu alilokuwa akipumzika na
kulala, mtemi Seneki Mwanakiyungi wa kabila la Wanyamwezi na kuacha
alama za makalio na mkuki sehemu hiyo.

Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya Mafunzo, kwa uandishi wa njia ya mtandao,
yaliyoandaliwa na UTPC na kushirikisha wanahabari 15, kutoka mikoa ya
Tabora na Singida, yaliyofungwa jana alhamisi, mjini Tabora.
 

Post a Comment