MAJI

| No comment yet
Na Vctor Kinambile

Wakazi wa mji wa Tabora wataanza kupa huduma bora ya maji baada ya kufungwa kwa mtambo mpya ambao unarajiwa kuwasili siku yeyote kunzia sasa.

Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa tuwasa meneja biashara wa mamlaka hiyo Bernad BIswalo,alisema kwamba kwa muda mrefu wakazi wa manispaa Tabora  wamekuwakipata huduma kwa kusua sua .
Alisema kwamba kusua sua huko kulitokana na mitambo ambaoyo inasababisha usukumaji wa maji kutoka katika bwawa na kuwasambazia wateja kuungua,.

Kuungua kwa mashine hizo kulisababisha huduma ya maji katika mji kusimama kwa muda wa wiki sasa hivyo kuingia kwa mtambo huo utasaidia urejeshwaji wa maji katika hali ya kawaida

Alisema mamlaka imejiagiza mita 5000 ili kuwafungia wateja 2000 ambao walikuwa hawana mita najingine zitafungwa kwa wateja ambao walikuwa na mita lakini kwa makusudi wakaziharibu.

Mita ambazo zitafungiwa wateja ni za plastiki ambazo mamlaka imeziagiza ili kuweza kupambana na wafanya biashara vyuma chakavu ambao wamekuwa wakiharibu miundo mbinu ya mamlaka.http://www.mjengwaglob.com/

Post a Comment