BAADHI ya wazee walioshuhudia enzi za utumwa |
Na Abby Nkungu/Emmanuel Michael,
Tabora,
Januari 26, 2012,
Makumbusho
MAKUMBUSHO ya taifa mkoani Tabora yanaonekana kutekelezwa na wizara ya Maliasili na Utalii nchini kutokana na kutokuwepo na barabara ya kuaminika na kukosekanaa na mandhaari ya kuvutia.
Waandishi wa habari 12 kutoka mikoa ya Tabora na Singida waliotembelea Makumbusho hayo jana, wameshuhudia ubovu mkubwa wa barabara inayoelekea eneo hilo kiasi cha magari kupata taabu ya kupita.
Aidha mandhari ya eneo hilo haijaboreshwa vya kutosha kulingana na umuhimu wa makumbusho hayo ya taifa ambayo hayana uzio na choo kwa ajili ya wageni wanaotembelea eneo hilo la utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari waliopo kwenye mafunzo ya siku nne juu ya uandishi wa mtandao, Mhifadhi msaidizi wa mambo ya kale bw Hamisi Mohamed Kaloka alisema kuwa licha ya ahadi lukuki za wizara kuboresha eneo hilo lakini hakuna kilichofanyika hadi hivi sasa.
Makumbusho hayo ambayo yapo umbali wa kilomita tisa hivi kutoka mjini Tabora barabara ya kuelekea Sikonge, ni muhimu kwa historia ya Tanzania kutokana na eneo hilo kuwa kituo kikuu cha kukusanyia watumwa kabla ya kusafirishwa.
Pamoja na kupumzikia watumwa, pia Mmisionari Dk David Livingstone aliishi katika eneo hilo kabla ya kuondoka kuelekea ujiji Kigoma.
1 comment
HILO DARASA LINAISHA LINI NYIE WA SINGIDA NA TABORA
Post a Comment